Skip to main content

Mistari ya Uponyaji ya Biblia

Tunapopitia changamoto nyingi mara nyingi tunahangaika sana na wakati mwingine tukisahau kuwa yupo Mungu yeye muweza wa yote, yeye aponyaye na kutakasa, tabibu wa matabibu. Hakika majina yote mazuri ni yake.

Hii ni baadhi ya mistari ya Biblia ya uponyaji, isome na ubarikiwe na kupokea uponyaji:-

Isaya 40:29

Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo.

Zaburi 147:3

Huwaponya waliopondeka moyo, na kuziganga jeraha zao.

Isaya 57:18-19

Nimeziona njia zake, nami nitamponya, nitamwongoza pia, nitamrudishia faraja zake, yeye na hao wanaomlilia. Mimi nayaumba matunda ya midomo; Amani, amani kwake yeye aliye mbali, na kwake yeye aliye karibu; asema Bwana; nami nitamponya.

Zaburi 103:2-5

Eeh nafsi yangu umhimidi Bwana, wala usizisahau fadhili zake zote. Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote, Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji ya fadhili na rehema, Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai,

Isaya 38:16-17

Ee Bwana kwa mambo hayo watu huishi, na uhai wa roho yangu u katika hayo yote, kwa hiyo uniponye na kunihuisha. Tazama nalikuwa na uchungu mwingi kwa ajili ya amani yangu, lakini kwa kunipenda umeniokoa na shimo la uharibifu kwa maana umezitupa dhambi zangu zote nyuma yako.

Hosea 6:1

Njoni tumrudie Bwana, maana yeye amerarua, na yeye atatuponya, yeye amepiga na yeye atatufunga jeraha zetu.

Mathayo 4:23-24

Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna katika watu. Na habari zake zikaenea katika Shamu yote, wakamletea wote waliokuwa hawawezi,  walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.

Asante kwa muda wako kusoma ujumbe huu, Mungu akubariki sana.

Comments

Popular posts from this blog

Jeff Bezos new girlfriend and future to be wife Lauren Sanchez random pictures yesterday event

 

Tazama Listi ya Nchi 10 Bora Zenye Warembo Wazuri Zaidi Afrika

Zifuatazo ni nchi 10 bora zenye warembo wengi na wazuri zaidi Afrika:- Ethiopia:   Ethiopia ni nchi yenye utajiri wa tamaduni na wanawake wenye sura za kuvutia. Wanawake wa Ethiopia mara nyingi wanajulikana kwa macho yao ya kupendeza na ngozi yao ya asili. Mfano maarufu ni Liya Kebede, mwanamitindo ambaye amekuwa ikoni ya urembo wa Ethiopia kimataifa. Wengine ni Sara Nuru, Gelila Bekele, Lola Monroe, na Helen Getachew, ambao wameendelea kuwakilisha urembo wa asili wa Ethiopia katika tasnia ya mitindo na burudani. Tanzania:  Tanzania ni nyumba ya utamaduni mchanganyiko na uzuri wa kipekee. Wanawake wa Tanzania wanajulikana kwa ngozi yao yenye rangi ya asili na tabasamu lao la kupendeza. Hamisa Mobetto, Flaviana Matata, Millen Happiness Magese, Irene Uwoya, Wema Sepetu, na Agness Masogange (Rest in peace) ni baadhi ya wanawake wenye urembo na vipaji kutoka Tanzania, wanaoendelea kufanya vizuri katika tasnia ya mitindo na burudani. Zimbabwe:  Zimbabwe ina wanawake wenye urembo wa asili na

Ali Kamwe Ataka Mpambano Mwingine na Mamelodi Sundowns

  Msemaji mkuu wa Young Africans (Yanga) amemuomba Rais wa Yanga Eng. Hersi Said kwenye kilele cha wiki ya wananchi kuufungua msimu wa 2024/2025 apambane awaletee Mamelodi Sundwns. Akidai kwamba bado hawajamalizana. Nimemuomba Rais wa Yanga @Caamil8 Kwenye Kilele cha Wiki ya Wananchi kuufungua Msimu wa 2024/25 Apambane Atuletee Mamelodi Sundowns Sisi na Wao Bado Hatujamalizana.. — Ali Kamwe (@AliKamwe) April 7, 2024